Hii inaitwa gori(chair), ni nondo inayokunjwa kwa ajili ya kutenganisha kitanda cha nondo cha juu na kile cha chini katika nondo za slab yenye vitanda viwili.
Kama hujaambiwa saizi ya kutumia kutoka kwenye ramani, tumia mm12.
Pia kama hujaambiwa uziweke umbali gani kutoka kwenye ramani, weka gori moja kwa kila mita moja ya eneo.
Mfano una slab yenye upana wa 4m kwa urefu wa 5m, mita za eneo ni 4×5 = 20m² , hivyo unaweka gori 20 katika eneo hili.