Angalia kwa makini utaona vifundo(ncha) vya ringi vimefungwa kwa mtindo wa mzunguko kuelekea juu.
Yaani tuseme hizo nondo za kusimama za nguzo ziko nne(za kwenye kona tu ndo tunaongelea), ukizipa namba 1, 2, 3 na 4, ncha ya ringi ya kwanza inafungwa katika nondo namba 1, ringi inayofuata ncha yake itafungwa nondo namba 2, ringi inayofuata ncha itafungwa nondo namba 3, ncha ringi inayofuata itafungwa nondo namba 4, ringi ya tano ncha yake itafungwa tena katika nondo namba 1, utafanya hivyo hadi umalize nguzo hyo.
Kwa nini tunatakiwa kufunga hivi?
~ Ili kugawa uzito vizuri na kuifanya nguzo kubeba uzito kwa usalama na kushusha katikanguzo inayofuata.
Tusipofanya hivi?
~Rudia kusoma hapo juu.