Tatizo la harufu ndani ya nyumba

Updated on September 26, 2024 in Maji Taka
0 on September 26, 2024

Moja ya sababu kubwa ambayo husababisha harufu ndani ya nyumba, ni mfumo wa maji taka kutokufanya kazi inavyotakiwa.

1) Kwenye masinki

2) Kwenye choo

3) Kwenye bomba za kutolea maji sakafuni

Chini ya hizi point huwa kuna fiting’i zinawekwa ambazo zimejikunja kama S au P lengo maji yabaki katika hiyo sehemu ili kutumika kama kizuizi cha harufu kutoka kwenye mfumo kuingia ndani.

Haya maji yasipokuwepo harufu ndani inajaa.

Kwa nini maji yanakosa hili eneo ?
~Matumizi ya maji kidogo
~Matumizi ya maji yasiyosahihi
~Matumizi mabaya ya choo, hasa tishu, tishu hunyonya kiasi chote cha maji toka eneo hili kwa njia ya kapilari.

 
  • Liked by
  • ujenzi_hfg5oq
Reply