Kwa nini UKUTA hupukutika?

Updated on November 23, 2024 in Ukuta
0 on November 23, 2024

Inasababishwa na unyevu utokao chini ya ardhi, kama eneo halina chumvi madhara yake yanaenda taratibu, na kama eneo lina asili ya chumvi basi madhara yake yataenda kwa haraka zaidi.

Nini kifanyike?
Ni kujenga inavyotakiwa.

Kujenga inavyotakiwa ndo nini?
Ni kujenga kwa kufuata taratibu na kanuni za ujenzi.

Ndo maana yake nini?
Katika suala la kuzuia ukuta usipukutike, kanuni ya ujenzi inatwambia tutumie DPC na DPM inavyotakiwa.

DPC ndo nini?
~Hiki ni kifupi cha maneno ya kiingereza ikimaanisha Damp Proof Course, kwa kiswahili inamaanisha ni tabaka linalowekwa kwa ajili ya kuzuia unyevu usipite.

DPM ndo nini?
~Hiki ni kifupi cha maneno ya kiingereza ikimaanisha Damp Proof Membrane, kwa kiswahili ni tabaka linalowekwa kuzuia unyevu usipite

Kuna tofauti gani kati ya DPC na DPM ?
~Tofauti ipo,

DPC huwekwa juu ya msingi wa mawe au juu ya msingi wa tofali au juu ya mkanda wa zege uliwekwa juu ya msingi au huwekwa juu ya zege la jamvi kabla kuweka mstari(kozi) wa kwanza wa tofali, ili tofali ya kwanza ikae juu ya mota ya simenti iliwekwa juu ya DPC. Iwekwe kwa kuzidi upande wa ndani na nje ili hata plasta inakuja kulala juu ya hiyo DPC, pia sehemu za kuunga hakikisha unaipishanisha kiasi kisichopungua 20 sentimita. Hii hufanyika ili kuzuia maji yatokayo ardhini kupanda na ukuta.

Material inayoweza kutumika kama DPC ni nyingi lakini zinazopatika kwa matumizi ni zile zilizo katika mfumo wa rola ya lami, kuna nzito, na kuna zile za laini na kuna saizi ya kati. Hufungwa kwa urefu wa wastani wa mita 10 na upana wa mita 1.

DPM huwekwa juu ya mchanga uliowekwa juu ya jiwe(hardcore) au huwekwa juu ya mchanga baada ya kunyunyuzia dawa ya mchwa. Ikishawekwa vizuri kwa kupishanisha inavyotakiwa unaweza kumimina zege la jamvi juu ya hiyo DPM.

Lengo la kuweka DPM ni nini?
~Kuzuia unyevu kuja katika sakafu.

Kwani unyevu kuja kwenye sakafu kuna shida gani?
~Shida ipo!

Usipoweka hii sakafu itakuwa ya baridi sana kipindi cha masika, inaweza kusababisha vitu kupata uvundo na kupelekea kuoza, inasababisha nyumba isifae kwa matumizi ya binadamu kwa sababu itakuwa ya baridi sana wakati wa masika na pia hata wakati mwingine kama utakuwa umejenga sehemu ambayo inakuwa na unyevu muda wote wa mwaka.

Hii iko kwenye mfumo wa rola ya karatasi nylon nyeusi nzito ambayo hupatikana katika duka la vifaa vya ujenzi tu.

Kujenga inavyotakiwa inawezekana | 0754 565 136

 
  • Liked by
Reply