Kuna umuhimu gani wa kupima udongo wakati wa ujenzi wa ghorofa?

Updated on November 21, 2024 in Udongo
0 on November 21, 2024

Katika ardhi kuna tabaka mbalimbali za udongo na kila tabaka lina uwezo wake wa kubeba uzito.

Ndo maana tunachimba mashimo kadhaa katika saiti katika kina flani ili tupate kuupima matabaka yote yaliyopatikana katika kima hicho ili tupate kujua uwezo wa kila tabaka.

Baada ya pale hesabu za jengo zinafanyika kuanzia juu hadi chini kupata uzito wa jengo utakaolala katika udongo.

Kutokana na uzito wa jengo unatumia pia majibu ya udongo ili kupata kujua nguzo ziwe na kima gani ndani ya udongo, kitako cha nguzo kiwe na saizi gani?

Bila kupima udongo kuweka kima cha nguzo au saizi ya kitako cha nguzo utakuwa unabahatisha!

 
  • Liked by
Reply