KANUNI YA UZITO WA NONDO

Updated on October 1, 2024 in Nondo
0 on October 1, 2024

Ukiangalia nondo kwenye ncha ina umbo la mviringo(au duara)

Eneo = pai.d² /4
Kanuni ya duara yenye kipenyo.
d = kipenyo cha nondo (saizi ya nondo, mm20, au mm12, n.k)

Ukubwa wake
V=AL, eneo x urefu
V = volume (ukubwa),
A = Area (eneo)
L = length (urefu)

Mass(uzito) = Volume x density
density ya chuma = 7850kg/m³
Mass = (pai * d²/4 )*L * 7850 kg/m³

Mita 1 = 1000mm, tubadili hiyo kipenyo isome mita badala ya mm.

Mass = (pai * d²/4 * 10^6 )*L * 7850 kg/m³
Mass = 3.14*d² * L * 7850 /4*10^6 kg

d itasoma m, m*m = m², L inasoma m,
m²*m = m³

Mass = 3.14*d² * L * 7850 /4*10^6 kg
Kwa nondo yenye urefu wa mita moja,
Mass = 3.14*d² * 1* 7850 /4*10^6 kg
Mass = 3.14*d² * 1* 7850 /4*10^6 kg
Mass = 0.00616225d² kg
Mass = d²/162 kg

Kwa nondo ya mita 12
Mass = (d² / 162)*12 = d² /13.5 kg

Wakati unaweka vipimo kwenye hii kanuni usingaike kujiuliza kwamba ile saizi ya nondo niweke kwenye milimita au kwenye mita. Kazi ya kubadili vipimo imeishafanyika, kama nondo ni milimita 10, wewe weka 10 endelea na hesabu zako, kama ni mm20, weka 20 endelea na hesabu zako.

 
  • Liked by
Reply