Jibu ni Ndiyo!
Jambo Muhimu ni kuzingatia kanuni, taratibu na sheria za ujenzi.
Taratibu za ujenzi zinakutaka uzingatie vipimo vifuatavyo:-
~Step iwe ndogo kuliko unene wa zege la msingi,
~Overlap ya zege la msingi Kwenye step iwe na kipimo kikubwa Kati ya hivi;
=> 300mm,
=> 2 x step.
Mfano:
Ukuta wa msingi ni wa tofali za kulaza(kimo 150mm),ili ujenge vizuri yafaa uongeze na unene wa mota kiasi Cha 20mm,hivyo step itakuwa mm170.
Tumeambiwa step inatakiwa iwe ndogo kuliko zege la msingi,hivyo zege la msingi litakuwa mm200,
Overlap tumeambiwa iwe kubwa kuliko 300mm au kubwa au sawasawa na step 2
Step 2 = 2×170 = 340mm
Kipimo kikubwa Kati ya 300mm na 340mm,ni 340mm.
Hivyo nikija pale kwenye step ulipo jenga tofali likaunga na zege ukuta kwa juu ukawa level na zege,nikichokonoa kwa ulalo(horizontal measurements) yafaa nipate 340mm kutoka uso wa zege mpaka uso wa udongo kwa upande wa ndani ya zege na sio kipimo kimoja sawasawa na unene wa zege ambao ni mm200.
Kwa nini ,kwa sababu hapa ndo nyufa itataka kutokea kwa sababu ya step kwa sababu uzito hautalingana, sehemu nyingine kozi nyingi sehemu nyingine kozi chache.