Je, Kuna Udongo Usiofaa Katika Ujenzi?

Updated on September 27, 2024 in Udongo
0 on September 27, 2024

______

Jibu ni Ndiyo!
______

Katika ujenzi, Udongo ni tabaka la ardhi ambalo msingi wa nyumba hukaa. Hufanya kazi ya kupokea uzito wa jengo na kuuhifadhi bila kuleta madhara katika jengo.

Kwa kuwa udongo unafanya Kazi kubwa hivyo tabaka hili linafaa kuwa imara katika majira na nyakati zote za mwaka.

Kuna Aina nyingi za udongo, zingine zinafaa na nyingine hazifai.

Moja ya Udongo usiofaa ni udongo Mfinyanzi.

Sababu:
~Udongo huu unabadilika kutokana na nyakati, wakati wa jua kali (kiangazi) hupasuka na wakati wa masika huziba zile nyufa zilizotengenezwa wakati wa kiangazi,hufanya hivi maisha yote. Kifupi ni kwamba udongo huu husinyaa wakati wa kiangazi na mara upatapo maji (masika) hutanuka.

Kwa hiyo:
~Kutokana na sababu hii,unapojenga kwenye udongo huu bila kuchukua tahadhari,wakati wa kiangazi nyumba hupasuka,wakati wa masika zile nyufa #katika huziba hivyo kusababisha nyumba kufuata kitendo kinachofanyika kwenye udongo.

~Kitendo hiki hufanya nyumba kuwa kwenye mwendo wa kuvunjwa vunjwa katika kipindi chote cha uhai wa nyumba yako.

Tufanye nini?
~Jitahidi sehemu yoyote ya jengo isiguse udongo huu.

Isiguse, ndiyo isiguse! Tunafanyaje sasa?
~Hakikisha unaweka tabaka la mchanga ambalo litatenganisha jengo na huu udongo,

Tabaka liwe na unene gani?
~Tabaka la mchanga Kama inaeezekana liwe na unene wa sentimita 30.

Hizo sehemu za jengo ni zipi?
~Upande wa nje na upande wa ndani ya msingi
~Sakafu yote(kabla ya kupanga mawe au kabla ya kuweka zege au kabla ya kuweka sakafu)

 
  • Liked by
  • Gemwaga Ndege
Reply