Je, Harufu Chooni Husababishwa na nini?

Updated on September 30, 2024 in Maji Taka
0 on October 1, 2024

Harufu ni hali flani inayochafua hali ya hewa, hali hii husababishwa na sababu mbalimbali.

Harufu mbaya chooni husababishwa na mambo kadhaa, moja ya mambo hayo ni:-
#Uchafu ~ Usafi ukiwa hafifu chooni husababisha harufu mbaya.
~Hivyo ni busara tena ni afya kufanya usafi wa kutosha chooni.

#Maji yanayozuia harufu kuisha(Water Seal)
Masinki yote ikiwamo masinki ya choo yametengenezwa kwa mfumo ambao maji hubaki muda wote kutenganisha baina ya ndani ya choo na ndani ya mfumo wa maji taka ili kuzuia harufu kutoka katika mabomba ya maji taka kuingia ndani ya nyumba.

Maji haya huisha kutokana na sababu mbalimbali,moja ya sababu hizi ni kama ifuatavyo:-
~Matumizi mabaya ya vitambaa(toilet paper) husababisha kunyonya maji haya na hatimae huisha,yaani kitambaa kinabaki kikiwa kimegusa maji huku kimerefuka na kugusa bomba kutokana na hali hii maji hunyonywa kutoka kwenye sinki kuja kwenye bomba na baadae kuisha,maji haya yakiisha au kufikia kimo flani ambacho kitaacha nafasi ambayo kwayo husababisha harufu kupenya kutoka kwenye mfumo wa maji taka na kuingia ndani.

~Sababu nyingine ya kumaliza maji haya ni evaporation ambayo hutokea nyakati za kiangazi,hivyo ni kuwa makini wakati wa kiangazi kuhakikisha maji hayapungui kwenye sinki.

~Sabau nyingine ni kutumia nguvu nyingi wakati wa kumwaga maji chooni(Momentum) wakati wa kutumia ndoo kumwaga maji baada ya kujisaidia kwa choo zile zisizo na flushing system ambayo hufanya kazi automatic, nguvu ikitumika hutengeneza hali ya maji yaliyotangulia kwenye sinki kuvuta haya mengi na kusababisha maji yote kwenda.

#Hata jikoni hali hii inaweza tokea

Ili ujenge inavyotakiwa tafuta mtalaam wa ujenzi ili akujengee au akusimamie nyumba yako.

 
  • Liked by
Reply