Hizi namba hutumika katika miradi ya ujenzi wa barabara hasa barabara za kiwango cha lami.
Kwa nini namba hizi?
Namba hizi hutumika ili kuonyesha kila kitu kilichopo katika urefu wa barabara hiyo na pia kuonyesha vitu vyote vinavyotakiwa kuwekwa au kujengwa katika urefu huo wa barabara husika.
Mfano miti inayotakiwa kutoka, nyumba zinazotakiwa kutoka, miundombinu inayotakiwa kutoka au kuhamishwa, mito au makorongo, au miamba au mawe yanayotakiwa kutoka.
Kuonyesha madaraja au makalavati yanakotakiwa kujengwa.
Vilevile kuonyesha kila eneo linatakiwa kujengwaje? Linachimbwa? kwa kiasi gani, linajazwa udongo kwa kiasi gani?
Namba hizi huanza mwanzo wa barabara hadi mwisho wa barabara.
Mwanzo wa barabara huitwa ziro ambayo hundikwa 0 + 000
Namba ya kushoto huonyesha kilomita na namba za kulia huonyesha mita. Unaenda ukiandika hizo mita upande wa kulia zinapotimia kilomita huamishiwa upande wa kushoto.
Mfano kwenye picha imeandikwa 2 + 622, inamaanisha kalvati hili liko umbali wa kilomita 2 na mita miasita ishirini na mbili kutoka mwanzo wa barabara.
