ELIMU KUHUSU MATUMIZI SAHIHI YA MAJI YA MITA

Updated on September 27, 2024 in Maji Safi
0 on September 27, 2024

Wengi hulalamika wanapoletewa bili ya maji pasipokujua MATUMIZI sahihi ya maji.

Hakikisha unapoletewa bili ya maji angalia usomaji uliopita(uniti za mwisho kusomwa), afu nenda kaangalie kwenye mita, je hizo uniti zilizoko kwenye bili ni kubwa kuliko uniti zilizoko kwenye mita? Au hizo unit kwenye bili ni ndogo kuliko zile zilizoko kwenye mita ?

1) Kama uniti za kwenye bili ni nyingi kuliko zile zilizoko kwenye mita jua kuna tatizo kwenye usomaji wa unit.

2) Kama uniti zilizoko kwenye bili ni ndogo jua bili inaweza kuwa sahihi.

UNASOMAJE UNIT KATIKA MITA ?
Mita ya maji ni Kama zile namba za pampu za vituo vya mafuta. Unasoma namba iliyoko kwenye kile kiboma, Kuna mita nyingine namba ya mwisho kulia ikizizunguka hadi kumi ndo namba nyingine za kushoto zinaongezeka. Kuna vile vijiduara vina mishale achana navyo vitakuchanganya.

Kila unit moja ni lita 1000 , kama hujui lita 1000, tafuta yale masimtanki yalipo angalia lile la lita 1000 ujue ndo unit moja au ndoo 50. Hivyo ukiambiwa mwezi huu umetumia unit 30 ujue umetumia lita 30,000 au ndoo 50*30=1500, wastani wa ndoo 50 kwa siku au uniti moja kwa siku.

Kwa kujua hivyo ndo uone je ni kweli unaweza kutumia ndoo 50 kwa siku? Kama jibu ni ndiyo utaona kama kuna uwezekano wa kupunguza matumizi ya maji, na kama huwezi tumia idadi hiyo na unit katika mita zinaonekana ziko mbele ya zile za mwisho kusomwa ongea na mhusika wa bill upate ufafanuzi.

KWA SIKU
Mtu mmoja anaweza tumia lita kuanzia 100 hadi 140 za maji kwa wastani kwa siku. Yaani ndoo 5 hadi 7 za maji kwa siku, hizi ndoo ni za lita 20.

Maji mengi hutumika wakati wa kuosha vyombo kama bomba liko sehemu ya kuoshea vyombo: unaosha vyombo huku bomba linamwaga maji.

kumwagilia bustani.
kuoga kwenye bomba la juu: unajisugua huku umeacha bomba linatirisha maji.

kufua kwenye sinki la kufulia nguo: kuacha bomba linatirisha maji wakati unafua.

kuosha gari.

kunawa mikono: wakati unaosha vizuri mikono na sabuni wakati huohuo bomba umeliacha linatirisha maji.

KWA SIKU
Kama wengi nyumbani hubaki kutwa nzima ujue matumizi ya maji yanongezeka, kama ni wachache wanabaki ujue matumizi ya maji yanapungua.

Sehemu za joto maji hutumika zaidi kuliko sehemu za baridi.

HAKIKISHA UNAKUWA NA KIDAFTARI UANDIKE UNIT KILA SIKU MFULULIZO HATA MIEZI 3, itasaidia siku ukiwa na malalamiko na pia itakusaidia kuona mwenendo wa matumizi ya maji nyumbani kwako.

 
  • Liked by
Reply