Pima maji na Pipe levo kipi nitumie?

Updated on November 28, 2024 in Vifaa Vya Ujenzi
0 on November 28, 2024

Vyote tumia lakini hakikisha kifaa unachotumia kinasoma ukweli hakipotezi.

Pima maji:
~Hiki kifaa kinahitaji umakini na utalaam wa kujua je maji yako sawa, kinasoma ukweli? Tofauti na hivyo utakitumia lakini jengo lako haliko wima.

Pipe levo:
~Hiki ni kifaa cha asili kinasoma ukweli mara nyingi,
LAKINI: Mtumiaji ahakikishe katika pipe maji yamejaa vizuri hakuna vinafasi ndani ya pipe, kukiwa na vinafasi(hewa au bubbles) pipe haitasoma ukweli.

Kama unataka kazi sahihi na ya uhakika tumia pipe levo.

 
  • Liked by
Reply