DPC ni kifupi cha neno la kiingereza DAMP PROOF COURSE, ikiwa na maana ya tabaka linalojengwa kwa ajili ya kuzuia unyevu utokao ardhini.
Inawekwa wapi?
Inawekwa juu ya mkanda wa zege wa msingi au juu ya msingi wa mawe au juu ya msingi wa tofali au juu ya jamvi kabla ya kuanza kujenga tofali la kwanza la ukuta wa boma.
Inawekwaje?
Hakikisha kwenye maungio inapishana angalau sentimita 20, na pia hakikisha inatokeza nje na ndani kiasi cha kutosha ili plasta ikipigwa ilale juu ya DPC, weka kuta zote. Isipowekwa inavyotakiwa ndo utasikia unaambiwa “DPC haizuii chochote unaharibu pesa yako”
Ikoje ?
Hii ni material ambayo kwenye mfumo wa rola ya lami. Kuna zile nzito na kuna zile nyepesi, katika hizi nyepesi kuna nyingine hazifai.
Ntaweza bei?
Ndiyo unaweza, uzuri unaingia gharama mara moja kwa maisha yako yote. Ukiona gharama kubwa ujue utaingia gharama nyingi za matengenezo kwa maisha yote ya hiyo nyumba.
DPM ni kifupi cha neno la kiingereza DAMP PROOF MEMBRANE, ikiwa na maana ya tabaka linalojengwa kwa ajili ya kuzuia unyevu utokao ardhini, inayowekwa eneo lote la sakafu.
Inawekwa wapi?
Inawekwa juu ya mchanga uliofunika mawe (hardcore) eneo lote la sakafu ya nyumba yako.
Inawekwaje?
Hakikisha kwenye maungio inapishana angalau sentimita 20, na pia hakikisha haitobolewi na mawe.
Ikoje ?
Hii ni material ambayo kwenye mfumo wa rola ya nylon ngumu huuzwa duka la vifaa vya ujenzi nyeusi. Kuna zile nzito na kuna zile nyepesi, nyepesi hazifai
Ntaweza bei?
Ndiyo unaweza, uzuri unaingia gharama mara moja kwa maisha yako yote. Ukiona gharama kubwa ujue utaingia gharama nyingi za matengenezo kwa maisha yote ya hiyo nyumba hasa ukiwa umejenga eneo lenye majimaji.