1 : Kuna yule anayefunga pazia katika grill za madirisha au frem za madirisjani.
~ Atakuwa amefunga pazia lakini kuna mapungufu mengi, pazia litakuwa limekaa vibaya, halijaziba dirisha zima.
2 : Kuna yule anagonga misumari ukutani halafu anafunga pazia.
~Misumari itakuwa inachomoka mara kwa mara, ukirudia kuweka unakuwa unaharibu ukuta.
3 : Kuna yule atoboa ukutani halafu anagonga vimbao baadae anafunga skrubu ndo afunge pazia.
~Vibao vitakuwa sio imara, hivyo mapazia yatakuwa yanadondoka mara kwa mara.
4 : Kuna yule anatoboa ukuta kwa mashine ya umeme, halafu anaweka fisha kwenye hivyo vishimo baadae anafunga vishika fimbo ya pazia baadae anapachika fimbo zenye pazia.
~Hii ndo njia sahihi ya uwekaji mapazia.
Kupitia somo hili utajifunza mengi kuhusu kufanya au kujenga inavyotakiwa. Hii inawahusu hata wakandarasi. Kuna wakandarasi wa namba 1, kuna wale namba 2, kuna wale namba 3, na kuna wale wa namba 4.