Kuna kanuni ya kukusaidia kupata uzito wa nondo yenye urefu flani. Tuangalie hiyo kanuni ilivyopatikana:
Uzito = Ukubwa * Denzite
Denzite(Density) ya nondo(chuma/steel) = 7850 kg/m³
Ukubwa wa nondo = eneo * kimo
Kimo = mita 1
Eneo = (pai * d² )/4
Hivyo,
Ukubwa = [ (pai * d² )/4 ] * 1m
d ni saizi ya nondo kwa milimita, tunataka iwe katika mita,
d = d/1000,[mita 1 = milimita 1000]
d = 0.00d(katika mita)
Ukubwa = [ (pai * (0.00d)² )/4 ] * 1m
pai = 3.14
Ukubwa = [ (3.14 * d² )/4 * 10⁶] * 1m
Ukubwa = 0.000000785 m³
Hivyo;
Uzito = ukubwa * denzite
Uzito = 0.000000785 * 7850 kg
Uzito = 0.00616 kg kwa mita moja.
Au
Uzito = d² / 162
Uzito huu unatakiwa uweke namba tu kwenye kanuni, mfano nondo saizi 12mm, weka tu 12.
Mfano uzito wa nondo ya milimita 12 yenye urefu wa mita 1 itakuwa na uzito ?
Uzito = (12 * 12)/162 = 0.888 kg
Kwa mita 12,
Uzito utakuwa = 0.888 * 12 = 10.66 kg
Tani moja ina uzito wa kg 1000
Hivyo idadi ya nondo kwa tani moja = 1000/10.66 = 93.8, tuseme 94.
Hivyo nondo yoyote unaweza pata uzito fasta bila shida na bila kupoteza muda.