Katika mfumo wa maji taka kuna mashimo makubwa mawili.
1 : Shimo dogo hili linatakiwa kuwa la mstatili.
Shimo hili lenyewe lazima lipigwe plasta, kwa nini linapigwa plasta ni kwa sababu lenyewe inatakiwa litunze kinyesi ili baadae likijaa gari ije inyonye.
2 : Shimo kubwa hili limegawanyika katika aina mbili, lipo lile ambalo linaitwa #soak_pit na lingine linaitwa #cess_pool.
~Kwa nini soak pit?
Ni soak pit kwa sababu linatakiwa liruhusu maji yanyonywe kwenda ardhini kupitia chini na kupitia mbavuni. Hili shimo hujengwa kwa kutumia mawe matupu bila saruji, na wakati mwingine unaweka saruji lakini unaancha matundu, ni vizuri ukaweka vibomba kwenye haya matundu ili kuhakikisha maji yanapenya vizuri.
Unaweza kujenga kwa tofali na kuacha matundu kama nilivyoelezea hapo juu.
Hakikisha unatumia matofali imara kwa sababu maji haya yanakuwa na kemikali inayokula sana tofali.
Mashimo ya aina hii huwa hayapigwi plasta, ukipiga plasta umeamua mwenyewe kufanya hivyo.
Pia mashimo haya hujengwa sehemu ambayo maji si mengi ardhini, pia udongo wa eneo hili huruhusu maji kupenya.
~Kwa nini cess pool
Haya ni mashimo ambayo hujengwa sehemu ambazo zina maji mengi ardhini, na sehemu ambazo maji hayaruhusu kupenya.
Haya mashimo yote hupigwa plasta, maji yakijaa gari itakuja kunyonya.
Je tusipopiga plasta itakuwaje? Maji ya nje yataingia shimoni, shimo litajaa, mfumo utashindwa kufanya kazi, nyumba itakuwa kero.
MUHIMU: Hakikisha mashimo haya yanakuwa mbali kutoka kwenye msingi wa nyumba, kama ukiweka karibu utadhoofisha uwezo wa msingi wa nyumba.