MFUMO WA MAJI TAKA

Updated on September 29, 2024 in Maji Taka
0 on September 29, 2024

Maji taka yana mfumo wake ambao huweza kufanya kazi inavyotakiwa bila kuleta madhara kiafya kwa wale wanaoutumia na pia kwa majilani.

Mfumo wa maji taka huanzia ndani hadi kufikia pale yanapotakiwa kuchakatwa,mashimo ya maji taka ya nyumbani,mashimo ya maji taka yaliyotengwa na mamlaka husika au Kama ni karibu na bahari huingizwa kwenye sewer kubwa inayotumika kuunganishiwa wote walioko jilani na hiyo pipe unakuwa unalipia Kama wanavyolipia maji Safi Ankara za kila mwezi.

Maji taka yanaanzia chooni,bafuni,jikoni na laundry.
Maji yenye sabuni hayafai kuchanganywa na maji yanayotoka chooni kwa kuwa sabuni itaua mfumo was uchakataji wa uchafu unaotoka chooni vivyo hivyo kwa uchafu unaotoka jikoni pia.

Maji taka yatokayo bafuni na jikoni huingia moja kwa moja kwenye shimo la mviringo Lile kubwa ili yakijaa yachotwe na gari la maji taka. Maji ya jikoni Yana mafuta ambayo hutanda juu na kuzuia hewa kuingia ndani ya maji taka,mafuta huelea kwa sababu Ni mepesi kuliko maji yaani density yake ndogo kuliko maji.

Mfumo wa maji taka huanzia kwenye masink Hadi chemba ndogo Hadi septic tank hadi soak pit au cess pool kupitia pipe zinazosaidia kusafirisha maji taka ,pipe hizi hutofautiana kulingana na ukubwa wa maji taka yanayozalishwa kutoka kwenye nyumba husika.

Baada ya kutoka Kwenye masinki kabla ya kuanza kuingia kwenye chemba ndogo,yafaa iwekwe pipe nje ya ukuta kwenye chemba ya kwanza ukutani,kazi ya pipe hii ni kuingiza hewa na kutoa kwenye mfumo ili kusaidia kupeperusha hewa nzito yenye harufu itokayo kwenye mfumo.

Pia pipe hii ni Kama pua na mdomo kwa binadamu, ukizama kwenye maji Kama hujui kuogelea lazima umeze maji aidha kupitia puani au kupitia mdomoni,ulimeza maji kwa sababu ulitaka kupumua lakini kwa kuwa uko ndani ya maji basi ukavuta maji.

Hata mfumo wa maji taka uko hivyo usipoweka bomba la kupumulia,hujawawi kwenda chooni ukakuta choo kimetapika,yaani kimerudisha maji taka ndani?

Baada ya kutoka kwenye chemba ndogondogo maji taka huingia kwenye chemba ya septic tank,hapa huingia kwanza sebuleni,ili kinyesi kichakatwe kishuke chini kwenye sakafu yabaki maji ili yaende chumbani tayari kwenda kwenye shimo kubwa. Hili shimo limegawanywa sehemu mbili ili kuzuia kinyesi kisiende kule kwenye shimo kubwa,ukuta unaogawa unajengwa lakini haufiki chini kwenye sakafu ili kuruhusu maji kupita,upande wa juu ukuta Huu lazima uzidi kimo kulinganisha na bomba linaloingiza maji.

Mambo yanayoingiza maji na kutoa lazima yatofautiane kwa kimo ,bomba la kutoa maji huwa chini kidogo ili kuzuia maji yasijekurudi ndani ya nyumba. Pia mabomba yote mawili lazima yafungwe “T” ili maji yashuke chini yanayoingia na maji yanayotolewa yaweze kuchukuliwa chini au ndani hivyo kuzuia kuchukua kinyesi ambacho hakijapita kwenye mfumo wa uchakataji,kwa sababu kawaida kinyesi density yake ni ndogo kabla hakijachakatwa.

Sakafu ya septic tank haiko level,imeinamia kule maji yanapoingilia.

Shimo kubwa yako ya aina mbili,Yale yanayopitisha maji sehemu ambazo water table haiko juu na udongo unaruhusu kusafirisha maji(Soak pit) na lipo ambalo hujengwa ili lisipitishe maji ,haya hujengwa sehemu ambazo water table iko juu au udongo haupitishi maji.

Mashimo ya maji taka kwa uchache kutoka kwenye nyumba yafaa iwe mita 3.

Ili kuzuia harufu ndani ya nyumba jitahidini kuhakikisha sinki limejenwa na #p au #s trap na kwamba maji yawe yamejaa inavyotakiwa.

 
  • Liked by
Reply