Ukaiangalia kwa makini utaona hizo nyufa ziko kama vibox, inaonyesha wire mesh zilitumika kwenye zege.
Sasa Kama zilitumika mbona !
Ni vizuri kutumia wire mesh kwenye zege la jamvi ili kuzuia nyufa na pia kuweka uimara katika kazi yetu.
Sasa mbona mesh zimetumika lakini kumetokea nyufa? Ndiyo mesh imetumika lakini ndivyo sivyo!
Kama unatumia mesh fanya hivi:
Gawa unene wa zege sehemu tatu, maana yake Kuna theluthi 3, ile theluthi ya juu weka mesh kwenye bottom, mfano zege la 150mm, ukigawa kwa 3 utapata 50mm, kutoka juu kwenye uso itakoishia zege, pima 50mm kwenda chini itakopishia weka mesh, maana kitachokuwa kimebaki ufike chini kabisa itakuwa 100mm
Zitakaaje? Weka magori zikae juu yao, je hazitabonyea wakati wa kukanyaga na zege, epuka kukanyaga watu wakiwa na zege au kutembeza toroli, weka mesh kidogo kidogo kwa kadri zinavyohitajika, kule zege linakotokea ndiko meshi ziwe zinafungwa kulifuata zege linakotokea.
Kwa nini tunaziweka upande wa juu? Tunaweka juu kwa sababu zege hili nyufa zake hutokea upande wa juu.