Mabati tunayotumia hutofautiana kutokana na mtengenezaji na lengo hasa la matumizi.
Mabati yana upana kuanzia 711mm Hadi 1067mm kutegemea na aina ya Bati.
Urefu wa Bati huanzia 2.0m,2.5m,3.0m na kuendelea Tena siku hizi unatengeneza makenchi na kuweka papi pamoja na fishabodi afu unapima unapeleka kiwandani wanaenda kukukatia kutokana na saizi jinsi unavyohitaji.
Mabati ya kawaida ya migongo midogo ya half round ,ukilifunika Bati ukihesabu utapata migongo 12.
Bati zikifungwa kwenye bando ,humo unakuta Kuna Bati dume,na Bati jike.
Mabati huchovywa kwenye madini ili kuweka tabaka la kuweza kuzuia kutu,Mfano zinc. Wakati mwingine hubandikwa vimchanga juu yake hii yote ni kuhakikisha Bati inadumu.
Ukilishika Bati ukalinyanyua utasikia Kama jepesi au zito,au ukiwa Kama unalikunja kwenye ncha utasikia gumu au jepesi,kama jepesi ujue namba ya gauge ni kubwa,Kama utasikia gumu au zito ujue namba ya gauge ni ndogo.
Kutokana na maelezo hapo juu:-
~Gauge 28 ni nzito au ni ngumu kuliko Gauge 30,
~Vivyo hivyo gauge 30 ni nzito au ni ngumu kuliko
Gauge 32.
Ndo maana Kwenye bando za Bati za Gauge 28 ni chache kuliko bando za Gauge 30(zenye urefu sawa)
Unene wa bati kutokana na Gauge ni Kama ifuatavyo:-
~Gauge 24 Bati zake Zina unene wa 0.7mm
~Gauge 26 Bati zake Zina unene wa 0.551mm
~Gauge 28 Bati zake Zina unene wa 0.475mm
~Gauge 30 Bati zake Zina unene wa 0.4mmm
~Gauge 32 Bati zake Zina unene wa 0.34mm.
Gauge ziko nyingi ila mara nyingi tunatumia gauge 26,28,na 30. Gauge 32 hutumika kwa matumizi ya ujenzi wa muda mfano uzio wa Miradi ya ujenzi (hording) au mabanda ya muda,na kwa wale wenye kipato kidogo kuliko kusubiri upate pesa ya kununua bati imara Bora utumie ya gauge ili upate sehemu ya kujihifadhi wakati huo unakusanya nguvu ya kupata mabati imara zaidi.