Maji katika zege yanafanya Kazi zifuatazo:
~Kusaidia saruji kuanza kufanya Kazi
~Kusaidia zege liweze kuwa rahisi kufanya nayo Kazi.
~Kuweka unyevu hadi zege likomae na kuwa imara
Maji katika zege yanaweza kuwa mengi, yaweza kuwa ya wastani au madogo zaidi. Kwa nini zege lingine linahitaji maji kidogo na zege lingine linahitaji maji mengi, hii inatokana uimara wa zege linalohitajika; Kama zege ni imara Sana linahitaji maji kidogo,Kama zege ni imara kwa wastani linahitaji maji ya wastani, na Kama zege hafifu basi linahitaji maji mengi.
Kwa nini yote haya, ntajuaje hili zege imara niweke kiasi flani?
Zege linahitaji maji na saruji kwa kanuni zifuatazo:
Maji/saruji = 0.45
Maji/saruji = 0.50
Maji/saruji = 0.55
Maji/saruji = 0.60
Hizo namba hapo juu zikiwa ndogo zinahitaji maji kidogo na ni zege imara, hizo namba kubwa zinahitaji maji mengi na zege lake sio imara Sana.
Maji yakiwa kidogo na saruji ikiwa nyingi hizo namba zinapungua. Maji yakiwa mengi na saruji ikawa kidogo hizo namba zinaongezeka.
Hivyo kwenye zege unahitaji:
~Maji/saruji = ?
~Uwiano(ratio) = ?
Hivi vitu viwili ndivyo vitakuongoza:
~Kiasi Cha maji utakochotakiwa kutumia
~Kiasi Cha saruji utakochotakiwa kutumia
Katika kila mita moja ya ujazo ya zege.